Chama cha soka nchini Uholanzi kimetangaza rasmi kuufuta msimu wa Ligi Kuu Uholanzi 2019/20 na hakutakuwa na Bingwa wala timu ya kushuka daraja.
Uholanzi wameamua kufuta msimu huo baada ya Waziri Mkuu wa Uholanzi kutangaza kuahirisha shughuli yoyote ya kimichezo hadi September 2020 sababu ya virusi vya corona.
Hata hivyo Uholanzi wamelazimika kufanya hivyo baada ya kuona kuwa hata wakisema wasubiri hadi September haitakuwa na maana kwani watatakiwa kuwa wameanza msimu mpya.