Kama hukusikiliza U Heard ya leo inahusu meneja wa Mapacha Watatu Khamis Dacota kushikiliwa Uwanja wa Ndege Zanzibar baada ya kutiliwa na mashaka.
Meneja huyo aliongozana na Wanamuziki wa Bendi hiyo ambao wao waliruhusiwa kupita ila yeye akazuiwa ambapo wahusika wa Uwanja huo wa Ndege walitilia shaka kuhusu uraia wake na aina ya vitu alivyovibeba kwenye mabegi yake.
Dacota alikaguliwa na Maafisa Usalama wa Uwanja wa Ndege kwa muda wa kama robo saa na baada ya kujiridhisha kuwa hakuwa na kitu chochote kibaya, walimruhusu akaondoka na wenzake.
Nimekurekodia hapa U Heard, unaweza kuisikiliza kwa kubonyeza play.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook