U Heard ya leo inamhusu mwanamuziki wa Bendi ya FM Academia, Patcho Mwamba ambaye kulikuwa na taarifa iliyoenea mitandaoni pamoja na picha kwamba amepigwa baada ya kufumaniwa na mke wa mtu ambapo yeye mwenyewe amekanusha na kusema kuwa picha hiyo aliiweka baada ya kupatwa na allege na aliiweka mtandaoni akiomba ushauri.
Baada ya hapo kukawa na story nyingine zilizosema Patcho ametishia kumuua mtu ambaye aliandika kwenye mitandao kwamba msanii huyo alipigwa baada ya kufumaniwa, kitu ambacho amekanusha kwamba sio kweli.
Kuhusiana na shutuma hizo Patcho amesema lazima amchukulie hatua za kisheria mtu huyo aliyemzushia kwamba amepigwa kutokana na kufumaniwa kwa kuwa amemchafulia jina lake kwa kumzushia taarifa za uongo.
Kuisikiliza U Heard hiyo bonyeza play hapa.
Hautopitwa na stori yoyote inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook