Story ya leo kwenye U Heard inamhusu msanii Hussein Machozi ambapo watu walimtumia ujumbe Soudy Brown kwamba msanii huyo amewaita Polisi na kuwakamata vijana kadhaa huko Mwanza.
Hussein amesema ni kweli kulitokea tafrani hiyo ambapo yeye alikuwa ukweni kwao Mwanza, wakaja watu na kuanza kutukana dirishani kwake bila sababu yoyote hivyo akaamua kutoa taarifa Polisi ili watu hao wakamatwe ajue sababu kwa nini walifanya vile.
Wakisaidiana na Polisi aliwakamata vijana wawili, lakini baadaye wakamalizana, Polisi wakaondoka.
Nilikurekodia U Heard ya leo iko hapa, unaweza kuisikiliza.
Hautopitwa na stori yoyote inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook