U Heard ya leo December 22 inamhusu msanii Ney wa Mitego ambapo story ni kwamba kuna taarifa za msanii huyo kwenda Kenya kwa ajili ya kufanya video ya wimbo wake mpya lakini kutokana na ratiba ya Director aliyehusika kushoot video hiyo kugonganisha ratiba ya Ney na Wizkid, ikabidi Ney asubiri kazi hiyo iishe ndipo ya kwake ianze ambapo ilifanyika chini ya kiwango hivyo Ney akaamua kuirudia video hiyo Dar na Director mwingine kutoka Kenya.
Ney amesema amefanya maamuzi ya kuirudia video yake kwa sababu Dar pia ina mazingira yote mazuri ya kufanyia video, hivyo akaamua kuirudia video hiyo na kwa sasa hayuko tayari kuzungumzia kuhusu kilichotokea.
Ney amesema kuwa video zote mbili zimemgharimu zaidi ya milioni 36, lakini kama ile moja angeridhishwa nayo gharama zake zisingefikia kiwango hicho.
Iko hapa U Heard ambayo nimekurekodia, unaweza kuisikiliza sasa.
Hakuna story itakayokupita mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook