Leo Novemba 18 kwenye show kubwa ya burudani Tz, XXL Soudy Brown a.k.a Gossip Cop kwenye U Heard ya leo meneja wa studio ya Bauncha Records Tito amelalamikiwa na msanii chipukizi Sadness ambaye amedai alilipa hela kwa ajili ya kurekodi nyimbo yake lakini baada ya kufanya malipo hayo, mtayarishaji huyo wa muziki hakumpatia kazi yake wala kumrudishia pesa aliyoilipia.
Baada ya kupigiwa simu meneja huyo Tito alisema anakumbuka msanii huyo alipelekwa na jamaa ambaye aliwaomba wamsaidie kurekodi na hakuna malipo yoyote waliyoyapokea kufanya kazi hiyo, hivyo kama msanii huyo alimpatia pesa mtu aliyemleta wao hazikuwafikia.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook