Muimbaji staa kutokea Marekani Demi Lovato ametumia ukurasa wake wa instagram kuelezea hali yake ya sasa na kushukuru mashabiki zake kwa mapenzi waliomuonyesha siku kadhaa zilizopita baada ya kulazwa hospitali kutokana na matumizi ya dawa za kulevya.
Kupitia ukurasa wake wa instagram Demi Lovato ameandika ujumbe huo ikiwa ni mara ya kwanza tokea alazwe hospitali July 24,2018 na kusema kuwa ataendelea kupambana na kuachana na matumizi ya dawa za kulevya.
“Nimekuwa muwazi kuhusu safari yangu ya matumizi ya dawa za kulevya , nilichojifunza ni kuwa ugonjwa sio kitu ambacho kinapotoea kwa muda, ni kitu nachotakiwa kuendelea kutatua lakini sijafanya hivyo bado”
Nataka kushukuru Mungu kwa kuendelea kuniweka hai na salama, kwa mashabiki zangu nawashukuru daima kwa mapenzi na mchango wenu kupitia wiki kadhaa zilizopita, mawazo yenu chanya na maombi yamenisaidia kuvuka katika kipindi hiki kigumu”
“Nahitaji muda na kutazama zaidi njia ya kupona, mapenzi mlionionyesha kamwe hayatosahaulika na ninatarajia siku amabyo nitasema nimetoka kwenye upande mwingine, nitaendelea kupambana”
MC PILIPILI kamtambulisha mke wake mtarajiwa, vipi Nandy na Nicole?