Mkurungezi wa TVE na EFM Majizzo amefanya mahojiano na Clouds TV kupitia kipindi cha Clouds 360 na kuzungumzia hali ya Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Fm Ruge Mutahaba ambaye bado yupo nchini Afrika Kusini akipatiwa matibabu.
Majizzo amesema kuwa kutokana na ukaribu alionao na Ruge Mutahaba alipokea kwa masikitiko taarifa za kuumwa kwake na atajitoa kupitia vyombo vya habari kwa hali na mali ili kuweza kuchangia kile alichonacho kwa ajili ya Ruge Mutahaba.
Haya ndio baadhi ya mambo ya msingi aliyoyaongea Majizzo kwenye kipindi cha Clouds 360.
” Undugu, urafiki na ukaribu wetu hauwezi kufa kwa sababu ya kazi zetu kwani ukitaka kuwa mfanya biashara mzuri hutakiwi kuchukulia vitu personal kwenye kazi huwa tunafanya kazi, na ili ukae muda mrefu kwenye biashara hutakiwi kuchukulia vitu personal na ukichukulia personal lazima upotee”
“Kabla sijafungua redio nilimwambia Ruge nataka kufungua redio akaniambia kwa sababu unaweza vitu vingi fungua, nilitaka kumfanyia surprise na nilivyofungua nikamwambia tayari nimefungua. Alinipongeza kwa furaha karibu kwenye game.”
“Nimepokea kwa masikitiko taarifa zake za kuumwa na kwa nafasi yangu nitaonyesha jinsi gani nimeguswa tutajitoa kwa namna yoyote kupitia vyombo vyangu vya habari au hata mimi personal, ili kuweza kusaidia hili kikubwa ni tuungane kwa pamoja”
‘Kamati ilikutana jana kwa bahati mbaya sikuwepo nilikuwa kwenye kamati zingine mipango haikuwa vibaya imekamilika, kamati yetu italeta mafanikio makubwa lengo letu ni kutaka Ruge arudi akiwa mzima, kikubwa ni ushirikiano pindi tukirudi kwenu wananchi’’
“Baada ya kupata taarifa za Ruge kuumwa, nilitamani miujiza ya haraka na nilikuwa najaribu kuweka karibu mawasiliano, na nilipata ushirikiano kutoka kwa watu wa hapa mjengoni na kunipa taarifa kuhusu hali yake”
“Kuna vitu vingi ambavyo tumepanga kuvifanya kwenye kamati yetu ya kihakikisha Ruge anarudi kwenye game na mwenyikiti wa kamati atakuja kuongea mengi ambayo tumeyapanga na mimi na vituo vyangu ( #TvE na #Efm) tutashiriki kwa pamoja”
VIDEO: Fid Q afikisha milioni 5 Salasala kwa Mama yake Godzilla