Liwezekanalo leo lisingoje kesho na hii imetokea kwa staa maarufu Marekani Chris Brown baada ya kuamua kumfollow aliyekuwa mpenzi wake miaka kadhaa iliyopita Rihanna baada ya kusikia tetesi kuwa staa huyo ameachana na mpenzi wake Hassan Jemeel.
Chris Brown na Rihanna waliwahi kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na kuachana mwaka 2013 na baadae Chris Brown kuanzisha mahusiano mapya na mwanadada Karruche Tran na baadae wawili hao kuachana mwaka 2015 .
Kupitia mtandao huo wa instagram staa huyo hajamfollow Rihanna peke yake bali amemfollow Christina Milian ambaye ni rafiki wa karibu wa Karrueche Tran, baada ya Chris Brown kuwa’follow wawili hao tetesi zinadai kuwa huenda akarudisha mapenzi kwa Rihanna au Karrueche.
Christina Milian na Karrueche Tran
Chris Brown tokea aachane na Karrueche Tran hajawahi kuweka mahusiano yake ya kimapenzi kwenye mitandao ya kijamii na wengi kudai kuwa aliumizwa na kitendo cha kuzaa nje akiwa kwenye mahusiano na Karrueche.
MPOTO AMKALISHA MAKAMBA/ SHOLO MWAMBA AONDOKA NA KIJIJI