Uingereza imekuwa nchi ya kwanza ya Ulaya kufikisha idadi ya watu 32,000 waliokufa kutokana na maradhi ya COVID-19 na kuifanya kuwa kitovu cha maambukizi ya Virusi vya Corona barani Ulaya.
Kiwango hicho cha vifo kimepita kile cha Italia ambako hadi sasa takwimu zinaonyesha kuwa watu zaidi ya 29,000 wamepoteza maisha kutokana na virusi vya corona.
imeelezwa kuwa upimaji wa virusi vya corona katika nchi hizo mbili ulikuwa wa kiwango cha chini.
Na inaaminika kuwa takwimu za Uingereza na Italia ni zachini kuliko idadi halisi, kwa sababu zinatilia maanani tu wale waliokufa baada ya kuthibitika kuwa na maambukizi ya virusi hivyo.