Serikali imesema haita mvumilia Mwalimu atakaye fanya vitendo vya ukatili Kwa mwanafunzi huku ikiwataka maafisa elimu kuwashughulikia walimu watakaobainika kufanya vitendo hivyo.
Rai hiyo imetolewa na kaimu Katibu mkuu TAMISEMI Vicent Kayombo wakati akizungumza na Maafisa elimu wilaya na mkoa na wakufunzi vyuo vya Elimu ambapo amesema ni aibu kuona Mwalimu anafanya vitendo vya ukatili kwa watoto wadogo
Amesema hivi karibuni imesambaa video ikimuonesha Mwalimu akimuadhibu mwanafunzi Kwa njia tofauti Muongozo wa Sera ya Elimu Jambo ambalo limezua taharuki Kwa Jamii.
“Sitarajii kusikia Mwalimu amefanya ukatili Kwa mwanafunzi huku afisa elimu wilaya yupo na mkoa yupo haileti picha nzuri lazima mkasimamie mienendo ya walimu kazini”
Kwa upande wake Venance Manori Kaimu Mkurugenzi Elimu Msingi amesema wanafunzi wa shule za Msingi ni watoto wanapaswa kuelekezwa Kwa upole bila kutumia nguvu ili waendelee kupenda shule.
Anasema Serikali inatumia fedha nyingi katika kugharamia elimu bila malipo hivyo walimu na wazazi wanawajibu kushirikiana kwenye malezi ili lengo la Serikali litimie.