Umoja wa Ulaya umeidhinisha chanjo yake ya tano dhidi ya ugonjwa wa Covid-19, wakati shirika la afya duniani likihimiza kuongezwa kasi katika kukabiliana na kirusi cha Omicron.
Jana Jumatatu, wakala wa dawa za Ulaya EMA iliidhinisha chanjo kutoka kwa kampuni ya dawa ya Marekani ya Novavax.
Novavax ni chanjo ya tano kuidhinishwa na Umoja wa Ulaya baada ya Pfizer, Moderna, AstraZeneca na Johnson & Johnson, tayari Umoja huo umetia saini mkataba wa kununua hadi dozi milioni 200 za chanjo hiyo ya Novavax.
Kampuni hiyo ya dawa imesema chanjo yake imeonesha ufanisi wa asilimia 90.4 dhidi ya ugonjwa wa Covid-19 wakati wa majaribio yake.