Kuelekea maadhimisho ya siku ya mwanamke duniani Wakili Suzana Senso ametoa elimu ya kisheria kwa wanawake ambapo amesema Sheria ya Mirathi inamruhusu Mwanamke kuandika Mirathi ili kupata haki yake ya kimsingi ili kuweka kumbukumbu sahihi za mali zake.
“Mwanamke anaweza kuwa na mali na akarithisisha ndugu zake, Sheria inasema hata kama umeolewa, ukifariki Mumeo hana mamlaka ya kumiliki mali zako mpaka mirathi itakapokamilika, anaweza kuwa ni Mumeo, Watoto au Wazazi wako wakarithishwa” Wakili Suzan Senso