Michezo

CONFIRMED: Man United watashiriki Champions League 2017/18

on

Baada ya kukosekana kwa Man United katika michuano ya UEFA Champions League msimu uliyopita kwa kushindwa kumaliza katika nafasi nne za juu katika msimamo wa Ligi Kuu England msimu uliyopita na kukosa nafasi ya kushiriki Champions League.

Usiku wa May 24 2017 Man United licha ya kushindwa kumaliza katika nafasi nne za juu katika msimamo wa Ligi Kuu England msimu huu, imefanikiwa kupata nafasi ya kushiriki michuano ya UEFA Champions League msimu ujao wa 2017/18 baada ya kuifunga Ajax ya Uholanzi magoli 2-0.

Man United wakefanikiwa kuifunga Ajax magoli 2-0 katika fainali ya michuano ya UEFA Europa League ambapo kwa kawaida mshindi hupata nafasi ya kushiriki Champions League moja kwa moja hata kama hajamaliza katika nafasi nne za juu katika Ligi Kuu England.

Mchezaji ghali zaidi duniani Paul Pogba ndio alifanikiwa kuifungia Man United goli la kwanza kabla ya muarmenia wa kwanza kuwahi kichezea Man United Henrikh Mkhitaryan kufunga goli la pili dakika ya 48, kama Man United asingetwaa Ubingwa wa Europa asingepata nafasi ya kushiriki Champions msimu ujao.

Unaweza kutazama mahojiano ya Mkurugenzi wa SportPesa na AyoTV baada ya kuingia mkataba.

 

Soma na hizi

Tupia Comments