Kuna ishu ambyo imepewa Headlines sana Magazetini toka wameanza kujitokeza Wagombea Urais wa CCM, swali jingine ni kwamba eti Rais JK ana mtu ambae anamuandaa kumrithi?
Majibu yako kwenye hizi sentensi 10 nilizomnukuu >>>”Mchakato wa Uchaguzi umeanza kwenye Vyama vya Siasa… Na sisi tumeanza mchakato kwenye nafasi ya Urais, watu wamejitokeza kwa wingi na ni nzuri kwa Demokrasia“>>> Rais Kikwete.
“Mmoja alinitumia message akasema umenisaidia sana kufika hapa naweza kushika hata hiyo nafasi yako, nipe baraka zako.. nikamwambia ‘goodluck‘ sasa sijui ataitumia hiyo goodluck yangu kusema mzee amenichagua mie!”>>>
“Mimi sina mtu wa chaguo langu, Chama kitatusaidia kupata Kiongozi mzuri na makini… Kama wanaogombea kwenye Vyama wataamua kupigana vikumbo mpaka kutumia na misuli itakuwa imezidi, itabidi Serikali kuingilia kati… lakini kwenye majukwaa watu kusema sisi ndio zaidi ya wale hiyo haina maneno wala haileti ugomvi“>>> Rais Jakaya Kikwete.
Hapa utamsikia Rais JK mwenyewe akijibu ishu hiyo.
Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.