Urusiimeituhumu Marekani na washirika wake kuratibu na kufadhili mtandao wa maabara za kibaolojia ya kijeshi nchini Ukraine ikiwa ni pamoja na majaribio ya virusi vya corona, kimeta, kipindupindu, homa ya nguruwe na magonjwa mengine hatari.
Rais wa Urusi Vladimir Putin ametoa tuhuma hizo wakati akihutubia juu ya hali ya mgogoro wa Ukraine na kusisitiza kuwa Pentagoni imekuwa ikitoa ufadhili wa kifedha na kutoa miongozo kwa Ukraine kuhusu maabara kadhaa.
Kinachofanyika sasa, amesema ni “kujaribu kuficha programu hizi za siri.”
Putin ameeleza kuwa mamlaka za Ukraine zimeeleza waziwazi nia ya kupata silaha za maangamizi ikiwemo mabomu ya nyuklia. “Kwa kuzingatia mtazamo wa uhasama mkubwa wa Kiev, mifumo kama hiyo ingetumika kulenga Urusi mara tu ingekuwa tayari,”.
Washington imekanusha tuhuma za kufadhili mtandao wa maabara za kibiolojia Ukraine.