March 6, 2016 Chama cha madereva na makondakta wa daladala Dar es salaam, kimetangaza rasmi kuafikiana na yale makubaliano kati ya Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Paul Makonda na wamiliki wa magari hayo kutoa huduma ya kusafiri bure kwa Walimu wa shule za sekondari kuanzia kesho March 7, 2016.
Ambapo kila mwalimu atatakiwa kuwa na kitambulisho maalum, akiongea na waandishi wa habari Mwenyekiti wa chama cha madereva Tanzania Shabani Mdemu amesema>>
‘Yametikea mambo mengi, kuna watu watuchora kwenye vyombo vya habari kamamakatuni watumwa, sisi hatuko hivyo..! mtu yeyote aliye kwenye ardhi ya Tanzania ni lazima athamini mchango wa Mwalimu ‘
‘Na kama kuna mtu anawazo lingine ambalo litakuwa na msaada basi badala ya kupinga lililoanzishwa awasilishe na lake lifanyiwe kazi, sisi kama Madereva na makondakta tumelipokea hili la Walimu kusafiri bure na kuliafiki’
Unaweza kuitazama hii video hapa chini yenye full stori…..
Hii ndio siku Dc Makonda alivyotangaza rasmi Walimu kuanza kusafiri bure Dar…
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE