Moja kati ya ahadi alizitoa Rais wa Marekani Donald Trump akiwa kwenye kampeni zake ni pamoja na kuzuia wahamiaji kuingia nchini humo ambapo ripoti mpya zimesema Donald Trump atasaini sheria ya kuzuia kwa muda vibali vya wahamiaji kutoka Iran na nchi nyingine sita.
Taarifa za baadhi ya maafisa wa bunge la Marekani (Congress) na mtaalamu katika Idara ya Uhamiaji zimeeleza kwamba Rais Trump leo Jumatano anatarajia kusaini miswada kadhaa ikiwemo ya kusimamisha kwa muda utoaji visa kwa raia wa nchi za Kiarabu.
January 25, 2017 Trump aliandika kwenye Twitter kwamba itakuwa siku kubwa kwa usalama wa taifa, pamoja na mambo mengine tutajenga ukuta.
https://twitter.com/realDonaldTrump/status/824083821889015809
Ufafanuzi uliotolewa umeeleza kuwa Trump anakusudia kuzuia kwa miezi kadhaa wahamiaji kuingia Marekani isipokuwa wale aliowataja kuwa ni wa “Jamii za wachache wanaodhulumiwa” hadi zitapopitishwa sheria kali na ngumu kuhusiana na uingiaji wakimbizi nchini humo.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, maombi ya vibali kwa raia wa Syria, Iraq, Iran, Libya, Somalia, Sudan na Yemen vitazuiliwa.
Vilevile katika ukurasa wake Twitter, Trump ameonesha pia msimamo wake wa kujenga ukuta kwenye mpaka wa pamoja wa nchi hiyo na Mexico na kusisitiza kuwa ujenzi huo utatekelezwa kwa namna yoyote.
VIDEO: Kutana na Mtanzania aliyepata kazi Marekani kwa Tajiri namba 1 Duniani Bill Gates, bonyeza play kwenye hii video hapa chini