Wanasema tembea ujionee, au tulia uletewe….. sasa leo kwenye kumbukumbu za utafiti tumekutanishwa na hii moja inayohusu Watu wenye nywele nyingi mwilini, huu ni utafiti uliofanywa na Dr. Aikarakudy Alias.
Utafiti huu unaonesha kwamba Binadamu kuwa na kiwango kikubwa cha nywele mwilini kunachangia kwa kiasi kikubwa kumfanya awe na akili nyingi na upeo mkubwa wa kufikiri.
Utafiti huu uliotazama kiwango cha nywele kwenye miili ya Watu na ufaulu wao darasani pia uwezo wa kutumia ubongo wao kuchanganua mambo ulithibitisha kuwa wenye nywele nyingi iwe ni mikononi, kifuani, miguuni na maeneo mengine ya mwili wengi ni ma-genius yani Watu wenye uwezo mkubwa kiakili.
“Mainjinia na Madokta wengi tulibaini wana nywele nyingi, hata Wanawake wenye nywele nyingi mikononi na sehemu nyingine nyingi za mwili tuligundua wengi wamefanikiwa kimaisha” Je unakubaliana na utafiti huu?