Miji/Nchi

Utafiti Mpya: Je ni nchi gani maskini zaidi Afrika?

on

Afrika ni bara ambalo tafiti kadhaa zinafanyika na zimeendelea kufanyika, Matokeo ya Utafiti wa Africa Wealth umeitaja Zimbabwe kuwa ndio nchi Maskini. Inatajwa kuwa wizi wa kura, ukosefu wa kuheshimu haki za umiliki, vurugu, kukosekana kwa uhuru wa Habari, ni baadhi ya sababu ya Taifa hilo kuanguka na kuwa la mwisho.

Ripoti ya tatu ya mwaka ya Africa Wealth inasema watu wanaoishi Zimbabwe ni maskini katika bara la Afrika kwa kuwa na wastani wa pato la mtu mmojammoja ni US dola 200  ambapo ni kiasi ambacho watumishi wa umma wanakipata.

Ripoti imeeleza kuwa >>>’haki za umiliki ni muhimu kwa kuwezesha kujenga utajiri, Nchini Zimbabwe wamiliki wa Biashara hawana uhakika kama biashara zao au mali zao bado ni zao, hii inajenga hali ya woga kwa yeyote kutojitokeza kuwekeza kwenye nchi hiyo 

Wakati Zimbabwe ikianguka na kuwa nchi maskini, kisiwa cha Maurtius kimepanda na kuonekana kuwa watu wake ni matajiri kwa hadi pato la US dola 21700 kwa utajiri wa mtu mmojammoja. Mafanikio ya Mauritius yamehusishwa na kupata haki za umiliki ambapo imeshuhudiwa watu matajiri wakihamia huko katika muongo uliopita.

Utafiti uliofanyika kwenye nchi 20, zote zimekuwa na ongezeko la pato kwa kipindi cha mwaka 2000 na 2015, kasoro Zimbabwe

bbbb

zimbabwe poor

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenyeTwitter,FB,Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAMTWITTERFBYOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments