Mzozo kuhusu ni nani atakayemrithi marehemu Mfalme wa Wazulu, Goodwill Zwelithini, sasa unaelekea mahakamani, vyombo vya habari vinaripoti.
Mke wa kwanza, Malkia Sibongile Dlamini, anapinga kutekelezwa kwa wosia wa mfalme uliomtaja mfalme ajaye – huku kukiwa na madai kwamba wosia wake wa mwisho huenda ulighushiwa.
Hatua hiyo ya kisheria inakuja siku kadhaa baada ya kifo cha Malkia Shiyiwe Mantfombi Dlamini Zulu.
Alikuwa ameteuliwa kushikilia wadhifa huo tarehe 24 mwezi Machi baada ya Mfalme Zwethilini kufariki kutokana na matatizo yanayohusiana na ugonjwa wa kisukari akiwa na umri wa miaka 72.
Lakini katika kesi ya kupinga uteuzi wa Malkia Mantfombi kama mrithi wa Mfalme, Malkia Sibongile alitaka mahakama kutambua ndoa yake na marehemu Mfalme huyo kuwa halali. Pia anataka kupewa asilimia 50 ya usimamizi wa nyumba zake.
MEI MOSI: “TULIKUJA NA MATARAJIO YAKUONGEZWA, HATA KWA PUNGUZO TUNASHUKURU”