Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Prof. Adolf Mkenda leo Mei 8, 2024 amewasilisha Bajeti ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2024/2025 Bungeni Mkoani Dodoma.
‘Takribani Shule 96 za Sekondari ikiwemo Shule 26 za Serikali na 68 Binafsi zimeanza utekelezaji ya mitaala ya amali kwa Mwaka 2024’- Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda
‘Serikali itaongeza Wito wa Ukusanyaji Uchakataji na utoaji wa takwimu za Elimu kwa kuunganisha mifumo yote ya takwimu za Elimu ya awali, msingi, Sekondari, ualimu,ufundi, na mafunzo ya ufundi stadi, Elimu ya juu, pamoja na mifumo ya upimaji na tathmini na kuandaa kitabu cha Taifa cha Takwimu Muhimu za Elimu (Basic Education Statistics in Tanzania- BEST)’- Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda
‘Serikali imeongeza idadi ya Vituo vya Elimu ya Sekondari kwa njia mbadala kutoka Vituo 168 hadi vituo 190 ili kuongeza dursa za kupata Elimu kwa Wanafunzi waliokosa Elimu kwa şababu mbalimbali’- Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda