Watu wanaokutwa na UTI mara kwa mara wanaweza kuwa na mawe kwenye figo, Daktari Bingwa wa Magonjwa ya mfumo wa mkojo katika Hospitali ya Benjamin Mkapa, Dkt Remigius Rugakingira, ameshauri watu wanaokutwa na UTI mara kwa mara wafanye uchunguzi wa kina kwani wanaweza kuwa na mawe kwenye figo.
Dkt Rugakingira amesema kuna baadhi ya bakteria kwenye mfumo wa mkojo ambao wanafanya utengenezaji wa mawe kuwa mkubwa “Mtu anayetibiwaa UTI mara kwa mara anaweza kuwa na bakteria wengi ambao wanatengeza mawe kwenye figo kwa hiyo, ni bora akafanya uchunguzi wa kina”
Amesema Hospitali ya Benjamin Mkapa wanaweza kuyabaini mawe hayo kupitia teknolojia ya vipimo ikiwemo CT SCAN na Utrasound na kuwa wanaweza kutibu tatizo hilo pasipo upasuaji kwa kuwa wana mashine ya Shock Wave Lithotripsy (SWL) ambayo ni mashine inayotumia teknolojia kuyeyusha au kuyaponda mawe na kuyatoa kwa njia ya mkojo.