Sherehe za utoaji wa Tuzo za Oscars za msimu wa 94 zilizokuwa zimepangwa kufanyika February 27, 2022 zimesogezwa tena mbele mwezi mmoja na sasa zitafanyika March 27, 2022 sababu ikielezwa kuwa ni janga la Virusi vya Corona.
Hii sasa itakuwa ni mara ya pili mfululizo kwa Tuzo hizo za Oscars kuahirishwa, na ratiba mpya imetoka ya matukio yote yaliyopangwa kufanyika kwenye ukumbi wa Dolby Theatre huko Hollywood & Highland Center ambapo kwasasa ukumbi huo umefungwa kutokana na janga hilo.
The Academy Awards (Oscars) Hufanyika kila mwaka na kampuni ya Academy of Motion Picture Arts and Sciences (AMPAS) kwa lengo la kutambua mchango wa taaluma ya tasnia ya filamu, wakiwemo waongozaji, waigizaji, na watunzi wa filamu.
DIAMOND PLATNUMZ ATINGA OFISI ZA CCM, “NIMEFARIJIKA KUONA RAIS SAMIA KAAMINI VIJANA”