Kwa mujibu wa mtandao wa The Root umeripoti kuwa taarifa zilizotoka usiku wa March 25,2019 ni kuwa wakili wa R.Kelly, Michael Avenatti alikamatwa siku ya jana kufuatia tuhuma za udanganyifu na kutaka kujipatia fedha kutoka kwenye kampuni ya NIKE, Avenatti anadaiwa kuwahi kukaa na mwanasheria wa Nike kwenye kikao kimoja na kuzungumza.
Inadaiwa kuwa Michael Avenatti aliitishia kampuni huyo na kusema kuwa atafanya mkutano na waandishi wa habari siku ya mashindano ya mchezo wa kikapu ya NCAA na atazungumza vitu kuhusu vibaya kuhusu nguo za michezo zinazotolewa na kampuni hiyo vinginevyo wamlipe dola milioni 25 sawa na zaidi ya shilingi bilioni 58 za Kitanzania.
Inaelezwa kuwa Avenatti alikamatwa kwa kosa hilo na makosa mengine na tayari kwa sasa ameachiwa kwa dhamana ya Tsh. milioni 700 ikiwemo pia kusalimisha hati zake za kusafiria ikiwemo ya Marekani na Italia.
VIDEO: USHINDI WA TAIFA STARS/ RUBY KUPATA MTOTO/ FLAVIANA NA RIHANNA