April 7 inaweza kuwa siku yako ya kuzaliwa au siku muhimu kwa yeyote wa karibu yako, pia inaweza kuwa siku uliyofanikiwa kupata kitu flani na ikawa ya furaha kwako lakini kwa Irene Uwoya sio hivyo.
Tarehe hii Tanzania inawakumbuka Mashujaa wawili ambapo wa kwanza ni hayati Sheikh Abeid Amani Karume ambaye alikuwa Rais wa kwanza wa Zanzibar na mwingine ni mwigizaji nyota wa Bongo Movie marehemu Steven Kanumba.
Mwigizaji Irene Uwoya ni mmoja wa wasanii ambao wamefanya sana kazi na Marehemu Kanumba ambapo haya ndio maneno yake ameyatoa April 7 “Kiukweli nakumbuka mambo mengi sana.. Kwa sababu Steve kwangu mimi alikuwa mtu muhimu sana amenifundisha vitu vingi sana.. isitoshe Steve nilikuwa namjua kabla sijaanza kuingia kwenye sanaa nakumbuka vitu vingi kweli.. alikuwa mshkaji wangu sana mpaka nimeingia kwenye sanaa amenionesha njia vitu vingi tu tumefanya“
“Kinachoniumiza zaidi kuna mipango tu mingi ambayo tulikuwa tumepanga na yeye kabla hajafariki.. siku chache kabla hajafariki tulikuwa wote tumekaa tumekunywa.. tumeongea vitu vingi sana vya maisha na vya maendeleo kwa ajili ya tasnia.. baada ya kama siku mbili nikasikia hiyo. Tarehe ya leo inanikumbusha sana marehemu Steve, kiufupi siipendi siku ya leo.“– Irene Uwoya.
Alisikika kwenye #AMPLIFAYA.. Kama hukumsikia unaweza kumsikiliza hapa mtu wangu..
millardayo.com ndio sehemu yako kuzipata story zote mtu wangu, unaweza kuwa karibu zaidi na mimi kwa kujiunga kwenye Facebook, Twitter na Instagram pia zitakufikia zote mtu wangu, jiunge hapa >>>twitter Insta Facebook