Baraza la Mitihani Tanzania ‘Necta’ limeeleza kuwa shule zote zinazofungiwa kuwa vituo vya mitihani kutokana na sababu za ukiukwaji wa kanuni za baraza hilo wakati wa mitihani ya kitaifa haimaanishi shule hizo zinafungiwa kabisa kufundisha bali zinafutiwa kibali cha kuwa vituo vha kufanyia mitihani.
Katibu Mtendaji wa NECTA Dr. Charles Msonde amesema shule hizo zinaedelea na shughuli zake za kufundisha wanafunzi kama kawaida lakini unapofika wakati wa mitihani Baraza na Mamlaka husika huwapeleka watahiniwa hao kwenye kituo kingine ili kufanya mitihani yao.
>>>”Tunapofungia kituo pale tunapoona kuwa kituo hicho sio salama tena mitihani kufanyika hapo kwani inawezekana kituo hicho kikatumika kusambaza mitihani nchi nzima na hivyo ni hatari kwa usalama wa taifa kwa ujumla.” – Dr. Msonde.
ULIPITWA? Rais Magufuli atinga kanisani kwa Wasabato Magomeni, awapa pesa
Hii je? Mali za zaidi ya thamani ya BILIONI 2 kupigwa mnada DSM