Kozi ya uongozi mdogo kundi la 01/18_19 katika shule ya mafunzo ya awali ya kijeshi RTS kihangaiko imehitimisha mafunzo ya porini kwa zaidi ya askari 2000 kufanya shambulio la kunuia la mchana , Lililohusisha mashambulizi ya Ndege, mizinga mikubwa, na silahaa za msaada za kombania.
Mkuu wa mafunzo na utendaji kivita jeshini Meja Generali Alfred Fabian Kapinga amesisitiza kuwa, nidhamu na utayari wa askari ni nguzo muhimu katika jeshi, mithiri ya uwanja wa vita, katika eneo la mlima simba Msata, zaidi ya askari 2000 kutoka jeshi la wananchi Tanzania wanahitimisha zoezi la kivita kwa kutumia silaha nzito za kivita katika zoezi la medani Exercise maliza shabaha.
Meja Generali Alfred Fabian Kapinga Mkuu Wa mafunzo na utendaji kivita jeshini jwtz
Ikumbukwe kwamba, kufanyika kwa mazoezi haya ni utekelezaji wa maagizo ya mkuu wa majeshi ya ulinzi nchini Generali venance Mabeyo ambaye aliwataka wakuu wa shule zote za mafunzo ya kijeshi kuendesha mafunzo yatakayo jenga uhalisia wa vita kwa askari
Injinia alieambiwa soma hiyoo na RC Mwanri akutana na Makamu wa Rais (+video)