Mshambauliaji wa kimataifa wa Hispania mwanye asili ya Brazil Diego Costa anayekipiga katika club ya Atletico Madrid ya Hispania, amekataa kufanya mazoezi pamoja na timu ikiwa imepita siku moja tu toka apewe taarifa kuwa club yake ya Atletico Madrid itamuadhibu kwa kumfungiwa mechi 8.
Diego Costa hivi karibuni LaLiga ilitangaza kumfungia mechi 8 kucheza baada ya kubaini kuwa alimtusi muamuzi wa mchezo wa Barcelona dhidi ya timu yao ya Atletico Madrid, Diego Costa alioneshwa kadi nyekundu dakika ya 28 ya mchezo na kwakuwa ripoti ya waamuzi zilionesha kuwa alimtukata refa Jesus Gil, LaLiga walitangaza kumfungia game nane ila baada ya club yake nayo kudaiwa kupanga kumchukulia hatua amegoma kufanya mazoezi na timu kwa mujibu wa AS.
Tukio hilo lilitokea April 6 2019 katika mchezo huo wa LaLiga ambao Atletico alipoteza, Diego Costa alilalamika akiwa anaamini kuwa alichezewa faulo ila kutokana na kutoa lugha yake ya matusi akajikuta kaoneshwa kadi nyekundu dakika ya 28 na kutolewa nje, kwa maana hiyo Costa msimu wake wa LaLiga ndio umeisha.
Simba na Yanga za kataa kuungana ili kucheza na Mabingwa mara 5 wa Europa League May 23