Mahakama Kuu ya Tanzania imeizuia Bodi ya Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF, Prof.Ibrahim Lipumba kufanya shughuli zozote ndani ya chama hicho hadi kesi ya msingi itakaposikilizwa.
Uamuzi huo umetolewa leo na Jaji Wilfred Ndyansobera ambapo amesema amezisikiliza hoja za pande zote mbili baina ya waombaji na wajibu maombi.
“Mahakama hii imeridhika na hoja za upande wa muombaji, hivyo inaamuru bodi mpya iliyofunguliwa isifanye shughuli zozote za chama hadi hapo kesi ya msingi itakaposikilizwa,”.
Awali Jaji Ndyansobera aliyatupilia mbali maombi ya upande wa wajibu maombi kwamba asisome maamuzi hayo kwa madai kuwa wanakusudia kukata rufaa juu ya maamuzi ya Jaji huyo kukataa kujitoa kusikiliza mashauri ya CUF.
Vigogo wa Tanesco wenye mashtaka 202 ya uhujumu uchumi walivyofikishwa mahakamani