Ku-trend kwa ua rose jeusi kwenye mitandao ya kijamii imekuwa kama ni kitu cha kawaida kwa watu wengi ambapo huenda kukawa kuna dosari katika mapenzi au kuachana kwa wapendanao basi watu hutumia ua rose jeusi kuwajulisha watu kuwa wameachana au kuna dosari katika penzi.
Baadhi ya mastaa wamekuwa waki-post pia ua hilo jeusi kwenye mitandao ya kijamii endapo panapotokea dosari kwenye mapenzi ila kwa upande wa muigizaji na miss Tanzania 2006 Wema Sepetu imekuwa tofauti ambapo amepost ua rose jekundu katika page yake ya instagram.
Wema Sepetu ameandika>>>A Red Rose is a Symbol of Love” akimaanisha “kuwa ua rose jekundu ni alama ya upendo”
Ulipitwa na Wema Sepetu alia na mashabiki “Mimi ninamoyo, siyo chuma”