Leo March 28,2018 story ambayo imechukua headlines ni kuhusu staa mkongwe wa muziki wa Hip Hop kutoka nchini Marekani DMX ambaye amehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela baada ya makosa ya ukwepaji kodi na kupewa miaka mitatu ya uchunguzi.
X aliongea na Jaji Jumatano akiwa New York City mahakamani na kusema kuwa yeye ni mtu mzima kufanya vitu anavyofanya na kukiri kuwa alikuwa hafikirii kufanya mambo aliyoyafanya.
DMX alikamatwa July 2017 akiwa na mashtaka 14 ya ukwepaji kodi na kuonekana kukataa makosa hayo na kulipa dhamana ya dola za Kimarekani 500,000 na baadae kukubali shtaka moja kutoka kwa makubaliano na mamlaka husika tofauti na hicho angehukumiwa kifungo cha miaka 44 jela.
“Nilipokuwa Mwanamuziki nilikuwa vizuri sana kuliko nilivyo Mbunge” Prof. Jay