Baada ya kukamatwa kwa Mtanzania Edward Erihard (31) Mkazi wa Dodoma akiwa na Wahamiaji haramu 20 Raia wa Ethiopia katika gari aina ya Land Cruiser V8 likiwa na bendera ya Chama Cha mapinduzi Ccm katika eneo la Minjingu mkononi Manyara
Leo hii Kamishna Msaidizi wa Uhamiaji Mkoani Manyara Philon Kyetema amezungumzia kukamatwa kwa wahamiaji hao huku akisema gari hilo,bendera pamoja na Dereva havina uhusiano wowote na Chama Cha Mapinduzi.
“Gari lilikuwa na mringoti na baada ya kufunuliwa ikakutwa bendera inayofanana na bendera ya Chama Cha mapinduzi maana yake ni kwamba huyu bwana Edward alijiandaa kuhadaa vyombo vya ulinzi na usalama ili visimtie nguvuni lakini tunashukuru askari Polisi wa Minjingu waliweza kumtilia shaka na kuzuia gari na ndani kukuta wahamiaji hao 20,gari linashikiliwa kituo cha Polisi pale na kesho tutawafikisha Mahakamani”
“Naomba kufafanua kwa Watanzania ninaomba wasihusishe gari hilo na bendera inayoonekana kwenye gari hilo haina uhusiano na Chama Tawala Cha CCM,hilo gari lenyewe,bendera yenyewe pamoja na Dereva hawana uhusiano na Chama Cha mapinduzi”