Mwanamuziki wa Congo Koffi Olomide ambaye amewasili Nairobi Kenya leo asubuhi ya July 22 akiwa na wanamuziki wake pamoja na dancers wake kwa ajili ya show, ameripotiwa kukamatwa baada ya kumpiga teke dancer wake wa kike wakati wakiwa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyata Nairobi.
Koffi Olomide amekamatwa nje ya studio za Citizen TV usiku huu baada ya video ya tukio la kumpiga dancer wake wa kike kusambaa katika mitandao ya kijamii, hivyo inspector Joseph Boinnet kuagiza askari polisi wamkamate mwanamuziki huyo mkongwe.
Kisa kamili kilichomfanya Koffi Olomide kufikia hatua hiyo bado hakijawekwa wazi, Koffi amewasili leo asubuhi ya July 22 akiwa na timu yake kwa ajili ya show inayotarajia kufanyika kesho July 23 2016 katika uwanja wa Bomas, taarifa zinaeleza Koffi amekamatwa na kupelekwa uwanja wa ndege kwa ajili ya kurudishwa kwao.
#KoffiOlomidé piétine l’une de ses danseuse à l’aéroport de #Kenya. Voici les Raisons- https://t.co/xmqzEcMURA… #DRC pic.twitter.com/556Qjet907
— The Voice Of Congo (@VoiceOfCongo) July 22, 2016
KAMA ILIKUPITA JOH MAKINI AKIELEZA NAMNA ALIVYOIKAMILISHA “PERFECT COMBO” NA CHIDINMA