Timu ya taifa ya Tanzania kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 maarufu kama Serengeti Boys bado ipo Libreville Gabon kwa ajili ya michuano ya Kombe la mataifa ya Afrika kwa vijana wenye umri wa chini ya miaka 17, Serengeti Boys wapo Kundi B lenye timu za Angola, Mali na Niger.
Shirikisho la soka barani Afrika CAF limeonesha kujali maisha ya timu hizo za vijana na kuingia gharama za kuwagharamia kama wanavyofanya kwa timu za taifa za wa kubwa,CAF kuhakikisha usalama wa afya za wachezaji, katika timu zote nane shiriki zimewekewa clinic ya muda katika hoteli iliyofikia.
Clinic zilizowekwa katika hoteli kwa mujibu wa jopo la madaktari wa timu ya taifa ya Tanzania Serengeti Boys zimegharimu kiasi cha zaidi ya Tsh milioni 50 lakini wakipewa pia na ambulace inayoshinda na kuongozana na timu popote wanapokwenda, clinic hiyo ipo ndani ya chumba cha hoteli ambapo kimebadilishwa kwa muda.