Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu inatarajia kutoa hukumu katika kesi ya kutoa taarifa ya uongo kupitia mtandao wa Facebook, inayomkabili Bob Chacha Wangwe, November 8, 2017.
Bob ni mtoto wa marehemu Chacha Wangwe, aliyewahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Tarime, mkoani Mara na Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA-Bara.
Hatua hiyo inatokana na Wakili wa utetezi, Dk. Onesmo Kyauke kumueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi kwamba wamefunga ushahidi wao wa upande wa utetezi katika kesi ambayo upande wa mashtaka ulikuwa na mashahidi sita, upande wa utetezi ulikuwa na shahidi mmoja ambaye ni mshtakiwa mwenyewe.
Kutokana na kufungwa kwa ushahidi huo, Hakimu Shaidi ameahirisha kesi hiyo hadi November 8, 2017 kwa ajili ya kutoa hukumu.
Awali, katika ushahidi wake, Bob amedai kuwa yeye hakuandika maneno ya upotoshaji wala hajawahi kufanya hivyo.
>>>”Mimi nilitoa maoni yangu kuhusu uchaguzi wa Zanzibar na kasoro zake za kidemokrasia kama Watanzania wengine na waangalizi wa uchaguzi huo walivyofanya.”
Katika kesi hiyo namba 167, Chacha Wangwe anatuhumiwa kwa kosa la kuchapisha taarifa za kupotosha katika ukurasa wake wa mtandao wa Facebook ambapo anadaiwa alitenda kosa hilo March 15, 2016 ambapo alichapisha taarifa iliyosema:“…Tanzania ni ambayo inajaza chuki wananchi.… matokeo ya kubaka Demokrasia Zanzibar ni hatari zaidi ya Muungano wenyewe…. Haiwezekani nchi ya Zanzibar kuwa koloni la Tanzania Bara kwa sababu za kijinga.”
ULIPITWA? DIWANI MWINGINE KAWAJIBU LEMA NA NASSARI, KATOA SIKU SABA