Mwanamuziki raia wa Canada, Justin Bieber (28) amefichua kuwa anaugua ugonjwa wa kupooza usoni baada ya matamasha yake kuahirishwa wiki hii.
Justin amethibitisha hayo kwenye video fupi katika ukurasa wake wa Instagram ambao una wafuasi milioni 240, kwamba hali hiyo ni kutokana na kugunduliwa kuwa ana ugonjwa unaoitwa Ramsay Hunt.
“Kama unavyoona jicho langu halikonyezi, siwezi kutabasamu upande huu wa uso wangu… Kwa hiyo kuna kupooza kabisa upande huu wa uso wangu,” amesema.
SABAYA AMTAJA RAIS SAMIA BAADA YA KUACHIWA HURU, “AMEFANYA KWA WENGI, ALIWEKA MFUMO”