Afisa habari wa zamani wa Yanga SC ambaye ni mkuu wa wilaya ya Arumeru kwa sasa Jerry Muro amerejea Dar es Salaam akiwa likizo na amekutana na waandishi wa habari leo na kuongea nao kuhusiana na masuala yanayohusu club yake ya Yanga.
Yanga kwa sasa haijapata matokeo mazuri kwa mechi nne mfululizo zilizopita na mashabiki wamekuwa wakilalamika hivyo Jerry amewataka waungane na kuendelea kuisapoti timu yao, Jerry hakusita kuwacharura watani zao Simba SC hususani swahiba wake Haji Manara.
VIDEO: ZAHERA AIPA UBINGWA SIMBA, AELEZA HATMA YA LUC EMAEL NDANI YA YANGA