AyoTV

VIDEO: Mapambano dhidi ya corona, Wizara ya afya yapokea tena msaada

on

Tanzania ikiwa bado kwenye vita dhidi ya virusi vya corona ambavyo vimepelekea shughuli mbalimbali duniani kusimama, makampuni mbalimbali yameendelea kuiunga mkono serikali katika mapambano hayo.

Kampuni ya vilainishi vya mitambo na magari ya Liqui Moly kupitia kwa Mkurugenzi wake Faraja Mkinga vimetoa msaada wa kuzifanyia service gari zote 34 zilizochini ya Wizara ya afya ambazo zinatumika katika mapambano dhidi ya corona.

Liqui Moly wametoa vilainishi vyenye thamani ya zaidi ya Tsh milioni 6 na kuvikabidhi kwa Mkurugenzi wa Kinga Wizara ya Afya Dr Leonard Subi kwa niaba ya wizara.

VIDEO: EXCLUSIVE: NI KWELI GSM WANATAKA KUINUNUA YANGA SC? WATOA MAJIBU

Soma na hizi

Tupia Comments