Baada ya kufanyika kwa tukio la kihistoria kwa Yanga na ulimwengu wa soka kwa Marais wawili wa Nchi mbili tofauti Rais wa Malawi Lazarus Chakwera na Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania kuzindua jezi za Club hiyo Ikulu.
Sasa Uongozi wa Young Africans walitangaza kupatikana kwa Jezi hizo mpya kwenye maduka ya GSM Mall na Maduka ya Vunja Bei.
Sasa hapa Mabibi na Mabwana tumempata Mbunifu wa Jezi hiyo mpya, Sheria Ngowi akieleza yale tusiyoyafahamu kuhusu Jezi hiyo mpya ya Yanga ya Msimu wa 2023/24.