Top Stories

VIDEO:Tukio lote la Rais Macron kupigwa kofi mbele ya Walinzi

on

Mhariri Mchambuzi wa siasa za Ufaransa Marc Perelman ameiambia France 24 TV ya Ufaransa kuwa tukio lililosababisha Rais Macron apigwe kofi na Mwananchi leo halikuwepo kwenye ratiba ya Rais, aliamua tu kushuka na kusalimia Wananchi waliokuwa wakimpungia.
Marc pia amesema wakati tukio limetokea Rais Macron alikua amechelewa kufika kwenye eneo la tukio alikotakiwa kuwepo lakini akaamua kusimama ghafla na kusalimia Wananchi hawa. Vyombo vya usalama vya Ufaransa vimesema tayari Wanaume wawili wamekamatwa kutokana na tukio hili, mmoja akiaminika kuwa aliyempiga kibao Rais Macron lakini Mwanaume wa pili aliyekamatwa hajajulikana ni nani hasa, tutaendelea kufatilia.

BIRTHDAY YA JOSEPH KUSAGA ATINGA CLOUDS NA FAMILIA YAKE, AOMBA WIMBO WA MBOSSO “NAUPENDA SANA”

Soma na hizi

Tupia Comments