Kama ulikuwa umetulia na unajua lugha hii basi Polisi wa uwanja wa kimataifa wa ndege wa Mwalimu Nyerere wametoa dili kwa yoyote anayejua lugha ya Ki-etnam kwa sababau bado wanamatafuta mkalimani kwa ajili ya kumhoji Don Van ambaye ni raia wa Vietnam aliyekamatwa na meno 65 na kucha 467 za Simba.
Thamani ya nyara hizo za serikali imetajwa kuwa ni Milioni 189.4,Raia huyo wa Vietnam alikamatwa na nyara hizo za serikali akiwa kabeba kwenye begi lake la nguo zikiwa zimefungwa kwenye mifuko ya mchele na kahawa.
Hii ni mara ya pili kwa Polisi hao kutangaza dili hili kwa yoyote anayejua lugha ya kivietnam.