Jeshi la polisi kanda maalumu ya Dar es salaam limepiga marufuku ngoma za kitamaduni ambazo zimekuwa zikifanyika nyakati za usiku kwenye maeneo mbalimbali Dar es salaam ikiwa ni muendelezo wa kukabiliana makundi ya kihalifu ambayo yamekua tishio kwa usalama wa raia.
Kufuatia kuibuka kwa makundi ya kihalifu kama Panya road na Mbwa mwitu ambayo wengi wao wanahusishwa na ngoma hiyo kwenye uporaji na upigaji wa watu, Kamanda wa polisi kanda maalumu ya Dar es salaam Suleiman Kova anasema ‘ni marufuku kwa ngoma yeyote ya asili kuchezwa nyakati za usiku’
Kamanda Kova anasema kufuatia operesheni inayoendeshwa dhidi ya vikundi hivyo vya kihalifu, mpaka sasa tayari wanawashikilia wafuasi zaidi ya mia moja ambapo pia watu wengi wamekuwa wakilalamikia vitendo viovu vinavyofanyika nyakati za usiku wakati wa ngoma hizo maarufu kama ‘vigodoro’ pamoja ‘baikoko’ na sasa jeshi la polisi limetoa onyo kali kwa watakaoendeleza hizi ngoma kuanzia sasa.
Story hii na nyingine zote millardayo.com ipo tayari kukufikishia kwa wakati popote ulipo, kaa karibu yangu kwa kubonyeza >>> Twitter Instagram facebook ili kupata kila kinachonifikiwa ikiwemo pichaz, video, stori na mengine yote ya hii dunia ambayo nitakua nakutumia kupitia mitandao hiyo ya kijamii.