Kampuni ya kiteknolojia ya Nchini Nigeria iitwayo Paystack imenunuliwa kwa zaidi ya Dola za Kimarekani MILIONI 200 ambazo ni zaidi ya shilingi za kitanzania BILIONI 460.
Waliolipa dolari yote hayo ni Kampuni ya Marekani ya iitwayo STRIPE ambayo pia ni Kampuni maarufu Marekani inayodili na teknolojia ya malipo, dili hili linaifanya kampuni ya Paystack kuwa Kampuni ya kwanza chipukizi ya Nigeria kununuliwa kwa pesa nyingi zaidi.
Paystack ni kampuni chipukizi (yaani startup) inayotoa huduma za malipo kidigitali na ilianzishwa miaka mitano tu iliyopita na Vijana wawili ambao walikua Marafiki kwa miaka mingi ambao ni Shola Akinlade na Ezra Olubi ambao wote umri wao ni miaka 35 sasa hivi na wamekua wakifanya shughuli zao Lagos kwenye Taifa hilo ambalo miongoni mwa Nchi za Afrika zilizowekeza nguvu kwenye sekta ya Teknolojia.