Mmalaka ya Afya ya Nigeria (Federal Ministry of health) imetangaza kugundulika kwa mgonjwa wa kwanza wa COVID-19, raia wa Italia anayefanya kazi Lagos ambaye siku za karibuni alirejea kutoka Milan, Italia.
Kwa sasa mgonjwa huyo yupo katika uangalizi wa kimatibabu mjini Yaba, Lagos na Serikali inafanya juhudi kuwatambua watu wote ambao mgonjwa huyo alikutana nao.
Virusi vya Corona vinazidi kuenea Duniani hali iliyofanya baadhi ya nchi kuzuia watalii kuingia nchini mwao ili kuepuka ugonjwa huo huku Tanzania ikidaiwa kuendelea kupokea watalii wengi raia wa China.
–
Jumla ya vifo vilivyotokana na Corona hadi sasa ni 2,858 na watu waliotambulika kuambukizwa ugonjwa huo Duniani ni 83,045.