Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa amesema kwamba Serikali imejipanga kuzalisha zaidi ya Barakoa Milioni tatu na nusu kwa mwezi ili kukidhi mahitaji ya Watanzania wote.
Hayo ameyasema DSM alipokua katika ziara ya kutembelea Viwanda vinavyozalisha Barakoa (face mask) na Vitakasa mikono (Hand sanitizer) ambapo kwa siku ya leo ziara hiyo imefanyika katika Kiwanda cha Uzalishaji cha Prestine, Kiwanda cha Uchapishaji cha Five stars na Kiwanda cha Uzalishaji Mafuta na Vilainishi cha Total.
Waziri Bashungwa ameeleza kwamba uzalishaji wa Barakoa za kutosha kwa sasa ni muhimu sana na Serikali inahakikisha kwamba Viwanda hivi vinapata malighafi ya kutosha ili viendelee kuzalisha vizuri.