Leo October 2, 2019 Nakukutanisha na Kijana Stewart Asajile maarufu kwa jina la Mbeya Boy anamiliki brand ya ya tshirt ya ‘Mbeya Boy’ ambayo imevaliwa na watu wengi maarufu nchini akiwemo, Masanja, Mbunge Sugu, Izzo Bizness, AY, Rayvanny na Amber Lulu.
Stewart anatueleza ili kupata mtaji wa kuanza ku-print tshirt ilimbidi akope hela kwa mtu ili atimize lengo lake.
“Niliazima hela kama elfu sabini hivi lakini wakati naenda kuprint waliniambia kiasi kiko juu zaidi, nilirudi nyumbani nikakaa kama wiki, nikatengeneza logo nikaweka kwenye simu sikui-post” Stewart