Michezo

Baada ya kutolewa Mapinduzi Cup, Simba yafanikiwa kulipiza kisasi kwa Mtibwa Sugar …(+Pichaz)

on

Baada ya wekundu wa msimbazi Simba kutolewa katika hatua ya nusu fainali ya michuano ya Kombe la Mapinduzi na Mtibwa Sugar ya Manungu Morogoro. January 16 katika mchezo wa Ligi Kuu walikutana tena, hiyo ilikuwa ni nafasi kwa Simba kulipa kisasi kwa Mtibwa Sugar au kuendeleza rekodi ya kupokea vipigo.

Simba ambayo ilikuwa inacheza mchezo wake wa kwanza wa Ligi Kuu toka ianze kufundishwa na kocha wake msaidizi Jackson Mayanja, ambaye kwa sasa anasimama kama kocha mkuu baada ya Simba kumfukuza kocha wake wa kiingereza Dylan Kerr siku kadhaa nyuma, Simba kupitia kwa  mshambuliaji wake wa kimataifa wa Uganda Hamisi Kiiza, walifanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 1-0.

DSC_0363

Goli la Simba lilifungwa na Hamisi Kiiza dakika ya 8 kipindi cha kwanza, goli hilo lilionekana kuwagawanya Mtibwa Sugar kwa kipindi cha kwanza, kwani Simba kwa kiasi kikubwa waliutawala mchezo, Mtibwa walijaribu kutafuta goli la kusawazisha kwa bidii kipindi cha pili, jitihada ambazo hazikuzaa matunda.

Matokeo ya mechi nyingine zilizochezwa January 16

  • JKT Ruvu 1 – 5 Mgambo JKT
  • Toto Africans 0-1 Tanzania Prisons
  • Stand United 1-0 Kagera Sugar
  • Mbeya City 1-0 Mwadui FC
  • Coastal Union 1-1 Maji Maji FC

DSC_0338

DSCF1375

DSC_0339

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye TwitterFBInstagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.

Tupia Comments