Licha ya kuwa Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania bara klabu ya Dar Es Salam Young African wapo Mauritius kukipiga na klabu ya Cercle De Joachim katika harakati zake za kuanza kuwania taji la klabu Bingwa Afrika, Ligi Kuu Tanzania bara imeendelea leo February 13 kama kawaida kwa michezo mitano kupigwa katika viwanja tofauti.
Simba walikuwa Shinyanga kumenyana na wenyeji wao Stand United chama la wana, katika mchezo wao wa 19 wa Ligi Kuu, Simba ambayo iliingia uwanjani ikiwa na kumbukumbu ya kuibuka na ushindi wa goli 1-0 katika mchezo wake wa mwisho katika uwanja huo dhidi ya Kagera Sugar iliyocheza wiki iliyopita, February 13 imefanikiwa kuendeleza rekodi yake ya ushindi.
Simba imefanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 2-1, shukrani kwa Simba ziende kwa Hamis Kiiza Diego, aliyefanikiwa kupachika goli zote mbili dakika ya 37 na 47, huku kwa upande wa Stand United goli la kufutia machozi lilifungwa na Pastore Atanus dakika ya 89, baada ya kutumia vyema kosa la beki wa Simba Emily Nimuboma ambaye alikosea kupiga mpira na kujikuta katoa assist kwa Atanus.
Kwa matokeo hayo Simba imetimiza jumla ya point 45 na kukaa kileleni mwa msimamo wa Ligi , ikiwa na jumla ya michezo 19. wakati Stand United wameendelea kusalia na point zao 29 na nafasi yao ya 5. Kwa sasa Simba inaviombea dua baya vilabu vya Yanga na Azam FC ambavyo vina mechi za viporo, hivyo kama vitafanya vibaya mechi zao za viporo vitashindwa kumtoa Simba kileleni.
Matokeo ya mechi nyingine za Ligi Kuu zilizochezwa February 13
- Mgambo JKT 0 – 1 African Sports
- Mbeya City 5 – 1 Toto Africans
- Ndanda FC 1 – 0 Majimaji
- JKT Ruvu 1-1 Kagera Sugar
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FBYOUTUBE