Leo June 8, 2018 NACTE imetangaza kuvifungia vyuo 20 nchini kwa kukosa sifa sasa Mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro ametoa maagizo kwa watendaji wote wa serikali katika wilaya ya Arusha kuhakikisha wanafuatilia vyuo vyote vinavyokiuka hatua ili vichukuliwe hatua.
DC Daqarro amesema “Viongozi wote wa Serikali wahahakishe Taasisi zote zinazohusika na Elimu ziwe zimesajiliwa, kozi ziwe zinatambulika ili mjue kama kozi zinawasaidia wananchi au lah! ili muwaepushe wananchi na kutapeliwa”